Kampuni ya Seven Star Energy Investment Group, yenye makazi yake jimboni Sichuan nchini China itatumia dola milioni 164 kutengeneza meli inayofanana kila kitu la meli kama ya Titanic (replica) iliyozama karne moja iliyopita.
Meli hiyo itajengwa na kampuni ya China Shipbuilding Industry Corporation na itatumika kupamba park ya kaunti ya Daying iliyopo Sichuan kwa kuegeshwa kwenye mto Qi nchini China.
Meli hiyo haitatumika kusafirisha abiria na watalii kwenye kina kirefu cha bahari kwakuwa si watu wengi wanaweza kuingia tena kwenye safari ya kufanana na Titanic ambayo haikukamilika. Badala yake meli hiyo itakuwa alama ya mzuka wa Titanic.
Shirika la habari la Xinhua limesema meli hiyo itatengeneza hali ilivyokuwa pale meli hiyo ya kufahari ilipogongana na mwamba wa barafu.
Ujenzi wa meli hiyo yenye urefu wa meta 270 unatarajia kumalizika baada ya miaka miwili.
Hii si mara ya kwanza kwa watu kutaka kutengeneza meli nyingine ya Titanic. Bilionea wa Australia, Clive Palmer alitangaza kutengeneza ‘Titanic II’.