Wafanyabiashara wa Soko Kuu Mjini Njombe Wamerejea Tena Kauli Yao ya Kuutaka Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kukamilisha Ukarabati wa Miundombinu ya Maji na Umeme Ndani ya Soko Hilo.
Akiongea na tovuti hii Sokoni Hapo Baadhi ya Wafanatbiashara Hao Wamesema Kuwa Kwa Muda Mrefu Wamekuwa Wakikabiliwa na Changamoto ya Ukosefu wa Huduma ya Umeme na Maji Hali Inayosababisha Soko Hilo Kuwa Chafu.
Wakielezea Suala la Usafi Ndani ya Soko Hilo Wamesema Kuwa Licha ya Kutoa Fedha Kwa Ajili ya Kuzoa Taka Lakini Bado Zoezi la Kuzoa Taka Hizo Limekuwa Likichelewa na Kusababisha Mlundikano wa Taka na Harufu Mbaya Inayohatarisha Afya za Wafanyabiashara na Wateja Wanaofika Sokoni Hapo Kwa Ajili ya Kujipatia Mahitaji Yao.