Mwanaume mmoja wa Australia alijikuta katika wakati mgumu baada ya mende mkubwa mwenye urefu wa inch 1 kuingia kwenye sikio lake wakati amelala usiku na kumsababishia maumivu.
Kuhusu alivyokuwa akijisikia wakati mdudu huyo akiwa ndani ya sikio lake, jaribu tu kufumba macho na uwaze jinsi unavyojisikia(ga) pindi hata sisimizi akiingia skioni. Helmer helmer ameiambia ABC kuwa baada ya kuhisi kuna mdudu ameingia katika sikio lake Jumatano iliyopita, alijipa huduma ya kwanza kwa kujaribu kumuondoa kwa kutumia vacuum cleaner na kujiwekea maji sikioni bila mafanikio.
Madaktari wa Australia waliompa huduma helmer ya kumtoa mende huyo sikioni mwake wamesema hawakuwahi kutoa mdudu mkubwa kama huyo katika sikio la mwanadamu. Baada ya kufikishwa hospitali mwanzoni walidhani ni mdudu mdogo na kuamua kumuwekea mafuta sikioni, hali iliyosababisha azidi kuzama ndani.
Baada ya kufikishwa hospitali madaktari walifanikiwa kumuondoa mende huyo, na kudai kuwa hakuna madhara yoyote yaliyojitokeza katika sikio la Helmer.