Chura ni mnyama mdogo sana ambaye binadamu hamthamini na wala kumuogapa,lakini Tembo pamoja na kuwa mnyama mkubwa kuliko wote wa porini anamhara sana chura licha ya udogo wake.
Tembo hata akitaka kunywa maji bwawani,mtoni au mahali popote pale,lakini akisikia sauti ya chura au vyura wanaimba,basi yuko radhi kufa na kiu yake kuliko kuingiza mkonga wake kwenye maji hayo yenye chura.
Tembo anapokunywa maji ambayo huyachota kwa mkonga wake na kuingiza mdomoni,anaweza kuchota pamoja na chura.Chura huyo huenda moja kwa moja kwenye tumbo la mnyama huyo.Kwa kuwa Tembo ana tumbo kubwa basi chura hujisikia kama yupo bwawani na huanza kuimba kama kawaida yake.
ENDELEA KUSOMA STORY HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kwa kufanya vile,Tembo hujisikia vibaya na kuanza kutafuta njia ya kumtoa yule chura kwenye tumbo lake.Hivyo huanza kujibamiza kwenye miti,magogo na kujitupa chini kwa nguvu ili mradi tu chura asiendelee kumghasi ndani ya tumbo lake.Matokeo yake Tembo huyo hujiumiza vibaya na wengine hufa kutokana na kujidhulu huko.
Ndio maana Tembo anamuogopa na kumuheshimu sana chura kutokana na kelele zake ndani ya tumbo lake.
Utalii hususani wa wanyamapori na ndege ni moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya nchi yetu.
TUSHIRIKIANE KUWALINDA WANYAMA NA KUYALINDA MAZINGIRA.
CHANZO: MALIASILI YETU