Kijana mdogo wa sasa anawaza kula bata, sijui wana maana gani bata ukimuangalia ni mchafu
mawazo yake ya ajabu ajabu fuatilia utaona. Siku hizi fasheni kuwa shabiki wa chama au
timu inayofanya vizuri kuliko kuyatafuta hayo mazuri ili tuwe na maendeleo. Na
unamkashifukabisa mwenzako kisa timu yako imeshinda jana, au chama chaka unaona
ndio kinajua kuliko kingine, hivi kwanini tusioneshane umwamba kwa kuwa hata na fire
extinguisher katika nyumba zetu za kupanga au tulizojenga? Kwanini usituite vijana
wenzako tuje shambani kwako kununua mananasi yaliyokuzidi kwa wingi ili upate fedha
na sie tupate mananasi, ni mtazamo tu lakini kuna mengine mengi.
Katika maisha yangu hadi nimefikia umri huu nawaza kuwa na hotel ndogo tu hata isiwe
na vyumba vingi lakini nashindwa kwa kuwa sikuwa na mipango iliyo na umakini, miaka 40
nawaza tu niwe na hiki niwe na kile. Lakini unakuta kijana mdogo wa miaka 26 tu akiwa
anamiliki hotel yenye akili ingawa si kubwa sana lakini unamuona kabisa kwamba ni mtu
anayewaza na wazo lake limezaa.Angalia hotel yenyewe ninayokuambia halafu utaniambia
ninachozungumza.
Napenda sana kuona vijana tukiwa na maendeleo, tena maendeleo ya kutoleajasho la njia
ya halali na si njia za panya kama wengi tunaoona na kusikiakuwa wamekamatwa,
wamefungwa, wameharibika akili na miili.
Huu ni wakati wa mabadiliko ya fikra na si kukaa chini na kuanza kulia kuwa wachina, sijui
wawekezaji wanje wanachukua nafasi zetu, tupambane kuweza kujiingizia vipato kwa
kuwekeza mawazo yetu, mitaji yetu, akili zetu, fedha zetu na uaminifu wetu katika shughuli
za maendeleo ya kifamilia hadi kitaifa.Maendeleo hayaji kwa kuaihidiwa na baba,
mama, kaka, mwanasiasa. Maendeleo yanakuja pale wewe unapozaliwa tu, umeletwa
kwa kusudi maalumu na si kukaa kijiweni au barazani na kunyoosha miguu kama mikia ya paka
huku unalalamika Fulani hafanyi hili, Fulani hafanyi lile. Tukimchagua Fulani ndio ataweza,
aisee unajidanganya ndugu yangu. Ukitaka kuamini hilo wewe endelea kukaa na kulalamika
na kuchagua viongozi wa kukupa maendeleo ndio utanielewa.Napenda kumpongeza kijana
huyu kwa kutumia mawazo yake, ndoto yake, ubunifu wake, na kufikia hapo kwa njia sahihi
aliyotumia. Napenda kumuambia kuwa “ Napenda maendeleo yako, ila utanisamehe natamani
kukuzidi”
Nikipata ruhusa nitaongea naye na atatufundisha njia alizotumia kufikia hapo alipo, vijana ni
wakati wetu huu sasa kubuni na kuiga mema yatakayotufanya tuwe matajiri kwa njia sahihi.
Nipo tayari muda wowote kuchangia mawazo ukiniomba katika mambo yenye tija na si
kuniletea hadithina ulalamishi. Nipo tayari kuwa na rafiki mmoja muelewa kuliko 100
wabovu, jifunze kutoka kwa walio endelea ili nawe uendelee.
Imeandaliwa na Buberwa Robert