Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na kujaa maji eneo kati ya stesheni za Godegode na Gulwe mkoani Dodoma na kuharibu tuta la reli, unasikitika kutangaza kusitishwa kwa muda huduma ya usafiri wa abiria kuanzia leo Ijumaa Januari 10, 2014 hadi itakapotangazwa tena.
Wasafiri wote wenye tiketi halali wafike katika stesheni walizokatia tiketi hizo kwa ajili ya kurejeshewa fedha kuanzia leo!
Aidha taarifa hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal Mafikiri.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Januari 10, 2014