Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

DK. SLAA AMKANA KADA ALIYETEKWA

$
0
0

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amekana na kusisitiza kuwa hajawahi kuwasiliana na Mwenyekiti wa chama hicho, Wilaya ya Temeke, Joseph Patrick ili kumshinikiza ajiuzulu uongozi.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema taarifa zinazotolewa na Patrick kuwa viongozi wakuu wa chama hicho walimlazimisha ajiuzulu nafasi yake, baada ya kubainika kumuunga mkono Zitto, ni za uongo zenye lengo la kupotosha ukweli wa mambo.

Alisema siku zote chama chake hakina utaratibu wa kufanya kazi moja kwa moja na wilaya kwa namna yoyote ile.

“Nimeshangazwa na uzushi na uongo unaosambazwa na Patrick, kwamba sisi viongozi wa juu tulimshinikiza ajiuzulu… napenda kuhakikisha kwamba katibu mkuu huwa hafanyi kazi na wilaya… hizi ni hila zilizopandikizwa tu,” alisema Dk. Slaa.

Alisema yeye kama mtendaji mkuu wa chama, hajawahi kufanya mawasiliano yoyote na kiongozi wa wilaya kuhusiana na jambo lolote.

ENDELEA  KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Alisema kwa taratibu zilizopo, katibu mkuu huwasiliana na viongozi wa kanda au mkoa ambao ndio wenye mamlaka kikatiba kufanya mawasiliano ya kikazi na wilaya za chama.

Alisema hata kama kuna maagizo ambayo yanatakiwa kufika wilayani, anachoweza kufanya yeye ni kuagiza kanda au mkoa ambao wanaweza kushughulikia masuala ya ngazi za wilaya.

“Si kweli uongozi wa chama taifa uliwahi hata mara moja kumwelekeza kiongozi yeyote wa ngazi ya wilaya kufanya jambo au uamuzi wowote, mimi ni muumini wa Katiba nazijua taratibu.

“Taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari zilipotosha ukweli, uongozi wa chama taifa hauna wajibu kikatiba kufanya mawasiliano ya kikazi moja kwa moja na wilaya, tunachoweza kukifanya ni kuwasiliana na kanda au mkoa ikibidi.

“Ni bahati mbaya huyo anayesema mimi katibu mkuu na mwenyekiti (Freeman Mbowe), tulimlazimisha aitishe vikao vya kujiuzulu, hasemi ilikuwa lini na wapi, anaishia kutoa shutuma tu zisizo na ushahidi, mwambieni awaonyeshe hizo barua na nyaraka zinazomtaka kujiuzulu, nadhani hizo ni hila zinatengenezwa.


 MATIBABU
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema chama chake kimegharamia matibabu yote ya Patrick baada ya kufikishwa Taasisi ya Mifupa Moi.

Alisema uongozi wa chama ulimtuma Mratibu wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Nickson Tugara kwenda MOI kumjulia hali, Patrick pamoja na kulipia gharama za matibabu yake.

“Mratibu wa kanda alipofika hospitalini alinipa simu nikazungumza moja kwa moja na mgonjwa (Patrick), ambaye alinihakikishia kwamba hali yake inaendelea vizuri na angehitaji kuondoka hospitalini kurudi nyumbani.

“Nilimwambia asitumie fedha zake, hata kama kuna dawa amekwishazigharamia atuonyeshe stakabadhi ili chama kimrudishie.

“Kimsingi tulitaka chama kichukue jukumu lote la matibabu yake na alinikubalia na kunihakikishia kwamba hali yake inaridhisha na anaweza kurudi nyumbani kwake,” alisema Dk. Slaa

 Kauli ya Patrick 
Patrick ambaye anadaiwa kutekwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili na watu wasiojulikana Januari 6, mwaka huu, alidai uongozi wa CHADEMA ulimlazimisha kumkana Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe vinginevyo angefukuzwa uanachama.

Akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), alidai Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Dk. Slaa walimwita na kumwambia aache urafiki na Zitto, la sivyo watamfukuza kwenye chama.

Aliendelea kudai kuwa, kwa nyakati tofauti walimwambia aitishe mkutano wa Kamati ya Utendaji ya wilaya, ili ajiuzulu au amkane Zitto.

Patrick alielezea mvutano huo uliendelea hadi mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo wakuu hao walimtuma kiongozi wa M4C aliyetumwa na Dk. Slaa, ili amuombe kwa mara ya mwisho ajiondoe kwenye chama. 

Mgogoro ndani ya Chadema
Chadema kimekuwa katika mgogoro na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Kabwe Zitto kwa madai kiongozi huyo anakisaliti chama kwa kuandaa waraka wa kukisambaratisha unaoitwa ‘Waraka wa Mabadiliko 2013.

Mbali na Zitto, aliyekuwa Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo tayari wamefukuzwa uanachama.

Hata hivyo, Zitto alifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo imetoa zuio kwa chama hicho au mtu yeyote kujadili uanachama wake hadi kesi yake ya msingi itakapomalizika.

MTANZANIA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>