KOCHA, David Moyes,amekiri kwamba kikosi chake cha Manchester United kina udhaifu mkubwa. Ametamka hivyo baada ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la FA (Jan 5)
Manchester United ilitupwa nje ya michuano kwa bao la dakika ya majeruhi lililofungwa na Wilfried Bony na kuifanya Swansea City kushinda 2-1 ikiwa ni mara yao ya kwanza kufanya hivyo Old Trafford baada ya miaka 83.
“Hiki ni kipindi ambacho mtu utapenda ufanye usajili wa wachezaji wapya,lakini je wachezaji tunaowahitaji wanapatikana Januari?” Alisema Moyes.
“Kuna muda nashindwa kupata jibu, kwasababu wachezaji tunaotaka waje hawapo Januari, si kwa sababu hatutaki kusajili. Nilichosema nitajaribu, lakini ukweli kuna shaka kubwa kwenye usajili wa mwezi huu.”Alisema
Moyes aliongezea kwa kusema amechukizwa na mwamuzi baada ya mchezaji Adam Johnson kuipatia klabu yake ya Sunderland adhabu ya penalty na hivyo kupoteza mchezo huo kwa mabao 2-1.