Pesa haiwezi kununua penzi. Lakini ‘likes’ inaweza. Kama utani vile, mzee mmoja nchini Yemeni ametaka apate likes milioni 1 kwenye ukurasa wake wa Facebook ili amuoze binti yake.
Salem Ayash, mtunzi wa mashairi kwenye mji wa Taiz, hajatoa muda maalum kwa muoaji huyo kukamilisha kazi hiyo ngumu ya kumtafutia likes baba mkwe wake. Kazi hiyo ni ngumu mno kwenye nchi hiyo yenye watu milioni 24 na watumiaji wachache wa mtandao.
Story hiyo imekuwa maarufu nchini Yemeni ambapo bloggers mbalimbali wamekuwa wakiwaomba watu walike page ya mzee huyo ili kumsaidia jamaa apate mke. Mpaka sasa ukurasa wake una likes takriban 35,000. “Hakuna mtu Yemen anaweza kumudu kulipa mahari tena,” alisema Ayash kuelezea kwanini hakutaka apewe dhahabu ama pesa.
Baba huyo pia anadai kuwa anataka kumuona mume huyo mtarajiwa wa binti yake anayejulikana kwenye vyombo vya habari kama Osama, anafanya jitihada kulipa waridi lake.
Hata hivyo, yupo tayari kupunguza masharti yake.
“Anaweza kutumia mwezi, mwaka au hata miaka miwili kukusanya idadi hiyo ya likes. Nikiona kuwa amejituma, niko tayari kulegeza na kuwaona wakioana kwa furaha,” alisisitiza.