Gari iliyokuwa imembeba muigizaji wa "Fast and Furious" Paul Walker ilikuwa ikikimbia mwendo kasi wa kilometa 160 kwa saa pindi ilipoanguka. Taarifa hiyo ilitolewa baada ya uchunguzi kukamilika. Mwili wa muigizaji huyo mwenye miaka 40 uliungua kiasi cha kushindwa kutambulika kwenye ajali hiyo iliyotokea November 30 mwaka jana.
Gari hilo lenye thamani ya $400,000, lilikuwa likiendeshwa na rafiki yake Walker, Roger Rodas, ambaye naye alifariki kwenye ajali hiyo ya Santa Clarita, kaskazini mwa Los Angeles, walikokuwa wameenda kuhudhuria hafla ya kuchangisha fedha za msaada.
Uchunguzi huo ulibaini kuwa hakuna aliyekuwa amekunywa pombe wala kutumia madawa ya kulevya wakati wakiendesha gari hilo.