Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TANESCO WAFUNGUKA KUHUSU TATIZO LA NGUZO KUANGUKA ENEO LA BAMAGA,BARABARA YA BAGAMOYO

$
0
0

 Mafundi wa Tanesco wakiwa kazini
Kufuatia tatizo la kugongwa na kuanguka kwa nguzo za msongo mkubwa zaidi ya tano katika Barabara ya Bagamoyo, Afisa Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud amefunguka na kusema kuwa mafundi wapo kazini ambapo umeme utarejea kuanzia saa 1:00 usiku.
 Fundi wa Tanesco akichimba shimo kwa ajili ya nguzo iliyodondoka leo
Akizungumza na mtandao huu muda mfupi uliopita, Badra alisema hadi muda huu polisi hawajanikiwa kuwakamata wahusika waliogonga nguzo moja na kusababisha nyingine kuanguka usiku wa kuamkia leo.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


"Tatizo ni kubwa lakini mafundi wetu wapo kazini. tunatarajia hadi ifikapo saa moja usiku umeme utawaka maeneo yote yaliyoathirika hasa Kijitonyama," alisema Badra akiliomba jeshi la polisi kuwakamata haraka wahusika wa tatizo hilo.
Usiku wa kuamkia leo dereva asiyejulikana aligonga nguzo moja ya umeme jirani na Chuo Cha Posta Kijitonyama iliyoangusha nguzo zingine tano na kusababisha mlpuko mkubwa wa moto katika Barabara ya Ali Hassa Mwinyi maeneo ya Bamaga.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>