Mmoja wa wafanyakazi katika ofisi ya Mhandisi wa manispaa ya Dodoma akitoa amri ya kuondoa kimoja ya vibanda vilivyojengwa kiholela katika stendi ya daladala Jamatini wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa vibanda vya wafanyabishara.
Mhandisi masaidizi manisaa ya Dodoma Luanda akitoa maelekezo kwa mama lishe waliopo katika stendi ya Daladala ya Jamatini kujenga vibanda sawa na vipimo vilivyowekwa sawasawa na utaratibu na sheria ndogo ndogo za manispaa hiyo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mwajuma Salum maarufu Bibi Ndonga (64) akimlalamikia kwa kumuonyesha Mhandisi msaidizi wa manispaa ya Dodoma Luanda stakabadhi ambazo amekuwa akilipia katika kipindi cha miezi miwili bila kukabidhiwa eneo la kuweka kibanda chake cha biashara na viongozi wa eneo hilo mhandisihuyo alifika kuona utaratibu uliotumika kujenga vibanda vya biashara.
Askari wa kutuliza Ghasia wakiwa na mtutu wa Bunduki kusimamia uhakiki wa vibanda vya wafanyabiashara katika stendi ya Daladala Jamatini Dodoma kama utaratibu uliyowekwa ulifuatwa wakati wa ugawaji na ujenzi.