Jake Schellenschlager wa Maryland, Marekani, mwenye miaka 14 alianza kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito akiwa na miaka 12.Mpaka sasa anauwezo wa kunyanyua vitu vyenye uzito mara mbili ya uzito wake, na ndoto zake ni kuja kuweka rekodi ya kunyanyua vitu vizito akiwa na umri mdogo.
Jake ameiambia Washington Post kuwa alianza kufanya mazoezi baada ya kumuona baba yake akifanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito katika garage ya nyumba yao, mpaka sasa hufanya mazoezi kila siku.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mpaka sasa Jake amefanikiwa kuweka rekodi ya mashindano kadhaa ya kunyanyua vitu vizito kwa watu wa umri wake, ikiwemo ‘Powerliftng Bench Press Championships’ iliyofanyika York, Pennsylvania.
Baba yake alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa sio vizuri kwa watoto wa umri mdogo kunyanyua vitu vizito, na kuongeza kuwa Jake hajawai kulalamika juu ya maumivu na huangaliwa afya mara kwa mara.