Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

FATAKI ZA MWAKA MPYA 2014 ZA DUBAI ZAVUNJA REKODI YA DUNIA

$
0
0
 
Fataki (fireworks) za kuupokea mwaka mpya (2014) zilizorushwa katika jengo refu kulilo yote duniani Burj Khalifa lililoko Dubai zimevunja rekodi ya kitabu cha kumbukumbu za dunia cha Guinness. Fataki zipatazo 500,000 zenye rangi tofauti tofauti kwaajili ya kuupokea mwaka mpya 2014 ziliandaliwa kwa takriban miezi mitano, mtandao wa Guinness World Records umeripoti.
Fataki hizo zilidumu kwa dakika sita kuanzia saa 6 kamili usiku wa 01/01/2014.

Jengo la Burj Khalifa Dubai wakati wa mchana
Waandaaji wa fataki hizo walilenga kuvunja rekodi iliyowekwa mwaka 2012 katika Golden Jubilee Anniversary ya Kuwait.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
Jumla ya computer 100 zilitumika kuleta muonekano wa fataki hizo za Dubai zilizoambatana na muziki uliotengenezwa maalum kwaajili ya shughuli hiyo (choreographed musical soundtrack).
Rais wa Guinness World Records Alistair Richards aliyesafiri kutoka Uingereza hadi Dubai maalum kwaajili ya kushuhudia fataki hizo wakati wa kuupokea mwaka mpya alisema, “The scale of this record attempt is truly impressive and will ensure all eyes are on Dubai”.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>