Diamond Platnumz na Wema Sepetu wameendelea kuliimarisha penzi lao kadri siku zinavyoenda. Uhakika wa kuwa wapenzi hawa wenye uhusiano wa ‘on and off’ wamerudiana kwa kasi, ulijulikana baada ya picha zao wakiwa Hong Kong kusambaa mtandaoni hali iliyopelekea kuzuka mgogoro mkubwa kati ya Diamond na mpenzi wake Penny ambaye kuna tetesi kuwa wameshaachana rasmi.
Wema akiwa jukwaani katika show ya Diamond siku ya Christmas
Tangu hapo Wema amekuwa haoni aibu kuonesha mapenzi yake kwa Diamond ikiwa ni pamoja na kupromote show ya Diamond ya Christmas.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kwenye show hiyo ya jana ndipo mambo yalipowekwa wazi zaidi ambapo Wema alikuwa mmoja wa watu waliopanda kwenye stage na kuongea na watoto waliokuwa wakishuhudia show.
Kwa mujibu wa Mtandao huu, Diamond alisikika akiuliz: Mnataka kumjua mchumba wangu”? Baadaye wakati akitaka kuimba wimbo wake ‘Ukimwona’, hitmaker huyo aliuliza tena: Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani,” na ndipo Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.
Katika hatua nyingine baada ya show hiyo, Diamond alichukua private jet na kuelekea Mwanza kwenye show nyingine ya Christmas. Bahati mbaya hakwenda na Wema.