ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Baadhi ya Makachero wa Polisi wakijadiliana jambo baada ya kuona Mwili huo.
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya Toyota Spacio likiwa limebeba mwili wa mtu aliefari ambaye alitambulikwa kwa Jila la Khalid Kitala (47) na kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya Kulevywa tumboni.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa walipata taarifa za kuwepo kwa gari hilo toka kwa wasamalia wema ambao waliliona njiani, ambapo inasemekana lilikuwa linatokea Mkoani Mbeya kuelekea Dar.
Polisi wa mkoa wa Morogoro waliweka mtego wao kwenye kituo cha Mikumi na hatimaye kufanikiwa kukamata gari hilo likiwa na watu watatu ndani (majina yao yamehifadhiwa),pipi saba za vitu vinavyosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.
Mwili huo ulipelekwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na pipi nyingine kumi na saba tumboni mwa Marehmu huyo na inasemekana mtu huyo alifariki akiwa Mbeya.
Watu wote watatu ambapo wawili wanahusika na gari hilo na mmoja ni mfanyabiashara wa Kariakoo wanashikiliwa na polisi huko Morogoro.