Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Akikabidhi zawadi waliotoa katika kituo hicho kwa Mama Mkuu wa Wa shirika la Masista wa Moyo safi wa Maria, Sista Flora Chuma.
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa (pichani), Jana amejumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro. Mrembo huo ameungana na warembo wengine wawili , akiwemo Miss Kanda ya Mashariki, Missa Clara Pamoja Sabra Islam Miss Morogoro 2013 . Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa. Aliongozana na Wazazi wake pamoja na ndugu jamaa na marafiki zake.
![]()
![]()
Watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha masista wa Moyo Mtakatifu wa Maria cha Mgolele mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja jana walipopata Ugeni Kutoka kwa Miss Tanzania, Happiness Watimanywa aliyeambatana na wakurugenzi wa Miss Tanzania pamoja na wazazi wake ndugu na jamaa wake wa Karibu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundega Akiwa na Katibu wa Miss Tanzania, Bosco Majaliwa jana walipoongozana na Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Alipotembelea Kituo cha Kulea watoto Yatima cha Mgolole Kinachomilikiwa na Masista wa Moyo safi Wa Maria Cha Mkoani Morogoro
Ndugu na marafiki wa Miss Tanzania 2013 waliomsindikaza Happiness Watimanywa alipotembelea kituo cha watoto yatima cha mjini Morogoro..
Miss Tanzania 2013, Hapiness Watimanywa Kulia akiwa na mama yake mzazi
Wazazi wa Miss Tanzania Bwana na Bibi Watimanywa katika picha pamoja na mtoto yatima wa Kituo cha Mgolele walipomsindikiza mtoto wao ambaye ni miss Tanzania 2013 Hapiness Watimanywa alipoenda kusherekea Sikukuu ya Chrismass pamoja na watoto hao jana ambapo amepata mapokezi mazuri kutoka kwa uongozi wa kituo hicho.
Miss tanzania 2013 Hapiness Watimanywa akiwa pamoja na wadogo zake wakiwa wamewabeba watoto katika yatima wa kituo hicho
CHANZO : MATUKIO BLOG