Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WANAUME WANAONYANYASWA NA WAKE ZAO WAONGEZEKA

$
0
0
Idadi ya wanaume wanaojitokeza kwenye vyombo vya sheria kushitaki namna wanavyonyanyaswa na wake zao imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Kaibu Kamishna wa Polisi, Adolphina Chialo, wakati akizungumza kwenye mkutano wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, ulioratibiwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo (WiLDAF).


Kauli mbinu ya mwaka huu kwenye maadhimisho hayo ni “funguka, tumia mamlaka yako, zuia ukatili wa kijinsia kuboresha afya ya jamii”


Alisema hivi sasa jamii imeelimika na imeamua kukataa kabisa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ndiyo sababu hata wanaume wameacha woga wa kwenda kuripoti vitendo hivyo ili wasaidiwe.


“Zamani ilionekana kama jambo lisilo la kawaida kwa wanaume kuja kulalamika na hawakuwa wakija kwa wingi kama sasa hivi ambapo wanakuja wengi na kwa kweli tunawasikiliza na kuwasaidia kusuluhisha matatizo yao,” alisema Chialo ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Alisema matukio ya ukatili wa kijinsia yamekuwepo kwa miaka mingi iliyopita ila hayakuwa yakionekana kutokana na ukimya wa waliokuwa wakitendewa ukatili huo tofauti na sasa ambapo wameelimimika.

Mratibu wa Shirika la WiLDAF, Judith Odunga, alisema kutokuwa na uswa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume ni chanzo kikubwa cha unyanyasaji dhidi ya wanawake.
“Ili kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake ni lazima kuzungumzia kwamba kutokuwa na usawa kati ya wanawake na wanaume ni chanzo cha ukatili dhidi ya wanawake,” alisema.

Aidha, alisema mitazamo ya kijamii inayopuuzia nguvu ya wanaume dhidi ya wanawake inachochea ukatili dhidi ya wanawake .

“Tangu utotoni jamii imetufanya tuamini kwamba mwanaume ni muhimu kuliko mwanamke na hivyo inakubalika mwanaume kumtawala, kumiliki na kumnyanyasa au kumtumia kama chombo,”

Alisema nguvu inayotokana na mila na desturi inaidhinisha wanaume kuwadhibiti wanawake kimwili, kiakili hali inayosababisha mfumo wa ukatili dhidi ya wanawake kubadili jinsi ya kutumia nguvu walizonazo kuwasaidia kujenga uhusiano mwema katika ngazi ya familia na jamii. 

CHANZO: NIPASHE 



Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>