Msanii wa filamu, Wastara Juma amewaomba Watanzania na wadau mbalimbali kuungana naye siku ya tarehe 28 December 2013 saa tatu asubuhi makaburini Kisutu jijini Dar es Salaam kwaajili ya kufanya dua maalum ya Sajuki
Wastara ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Facebook.
“28 Jumamosi kuanzia saa 3 asubuhi naomba mashabiki wangu na wapenzi wa kipenzi changu kipenzi chenu Sajuki tukutane kaburini kisutu kwa ajili ya dua ya pamoja…kwa Dar es salaam lakini dua rasmi ni 2.01.2014 Songea, aliandika Wastara.