Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

KASEJA, MANJI WAWAFARIJI MASHABIKI YANGA

$
0
0
KIPA wa Yanga, Juma Kaseja amesema kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne kulichangia kupunguza ufanisi wake uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi iliyomalizika kwa Yanga kubugizwa mabao 3-1.
Hata hivyo Kaseja amewaomba mashabiki wa Yanga, wasiwe na hofu kwani atarudi katika hali yake ya kawaida na wale wote wanaombeza au kumtabiria mabaya wataona aibu na kunyamaza.
Wakati Kaseja akisema hayo, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewatetea kipa huyo na kocha Ernest Brands na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu kwa madai kuwa mechi yenyewe ilikuwa bonaza.
Akizungumza na HabariLeo Dar es Salaam jana, Kaseja alisema amesikitishwa na kipigo ambacho Yanga ilikipata kutoka kwa Simba juzi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, lakini watajipanga na wachezaji wenzake kuhakikisha wanafanya vizuri mechi za mzunguko wa pili Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa mwakani.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYAA HAPA CHINI


“Nimeumia sana kufungwa mabao 3, lakini hakuna jinsi hata mazingira ya bao la tatu nililofungwa, nilikuwa nje ya eneo langu la kujidai nikataka kuusogeza kwenye eneo langu ila ukabana katika miguu, nikateleza, jamaa (Juma Awadhimfungaji wa bao la tatu la Simba) akaupitia akaenda kufunga.
“Imeniuma sana, lakini sikuwa na jinsi, kwani nilikuwa nje ya uwanja tangu Juni mwaka huu, hilo nalo limechangia kiasi fulani kupunguza ufanisi wangu, ila sasa nitarudi kwa nguvu zote na nitawapa raha Yanga. Wale wote wanaoniombea mabaya na kugeuka watabiri kwamba sitang’ara watanyamaza,” alisema kipa huyo.
Alisema yapo makosa ambayo waliyafanya katika mchezo dhidi ya Simba, hivyo ni jukumu lao kurekebisha dosari hizo ili michezo mingine ijayo wasizirudie.
Yanga ilimsajili Kaseja kama mchezaji huru dirisha dogo la usajili lililoanza Novemba 15 mwaka huu, baada ya kipa huyo kumaliza mkataba wake na Simba Juni mwaka huu na klabu hiyo kuamua kutomuongeza mwingine na tangu wakati huo hakuwa na timu.
Suala la kukosa timu ya kuchezea lilimfanya Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kumuengua katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kilichoshiriki michuano ya Chalenji iliyofanyika Nairobi, Kenya hivi karibuni.
Kaseja alijiunga na Simba mwishoni mwa mwaka 2002 akitokea Moro United na aliichezea hadi mwaka 2008 alipojiunga na Yanga, alikocheza ligi ya mwaka 2008/2009, kisha akarejea Simba msimu uliofuata aliyomaliza nayo mkataba Juni mwaka huu.
Kwa upande wa Manji, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Yanga inacheza kama timu na kama kuna tatizo lolote ni tatizo la timu kwa ujumla wake huku akiwataka watambue kuwa yeye ndio anatakiwa kulalamikiwa na sio mtu mwingine.
Alisema kuwa Kaseja wakati akichezea Simba aliwahi kufungwa na Yanga lakini hakukuwa na malalamiko ya Simba kutaka kumuondoa.
“Mimi nashindwa kuelewa kuwa kuna watu ambao wanasema kuwa hawa watu hawatakiwi tatizo sio wao tatizo ni kwamba hata sisi hatukupata muda wa kujiandaa vema,”alisema Manji.
Akilifafanua zaidi hilo la kujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo, Manji alisema kuwa kwa muda mrefu wachezaji wake walikuwa wakiichezea timu ya taifa na hivyo hawakuwa na muda wa kukaa pamoja.
Alisema kuwa alilitambua hilo lakini hata hivyo aliwaruhusu kucheza mchezo huo kwa kuwa aliona kama asingefanya hivyo wadhamini ambao ni Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) wasingemwelewa.
Hata hivyo aliipongeza Simba kwa ushindi huo na kuongeza kuwa atajitahidi kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa Yanga haifungwi tena na Simba.
Aidha, Manji alionekana kukerwa na hoja zilizokuwa zikitolewa na Mzee Akilimali ambaye anajulikana kama mmoja kati ya wazee wa Yanga ambaye juzi alitoa lawama kwa uongozi kumsajili Kaseja akidai tangu mwanzo Baraza la Wazee liliuandikia barua uongozi kupinga usajili huo.
Manji alisema: Kuna mzee mmoja amekuwa kila kitu kuhusu Yanga yeye ndio msemaji akijidai kuwa ana machungu sana na klabu hii, hii sio sawa na hatakiwi kuendelea na hali hiyo”.
Hata hivyo alikiri kuwa Mzee huyo alimwandikia barua kumtaka asimsajili Kaseja lakini hata hivyo alieleza kuwa hakuitilia maanani barua hiyo kutokana na kutokuwa na umuhimu.

HABARI LEO

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>