Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

FANYA VITU KWA USAHIHI NA SIO VITU SAHIHI TU

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Inawezekana unaanza kushaangaa kuna tofauti gani kufanya vitu kwa usahihi na si kufanya vitu sahihi tu. Hiki kitu inawezekana umekutana nacho kazini kwako au siku moja utakutana nacho katika majukumu ya kila siku hapo ofisini.

Mara nyingi watu tunapenda kufanya vitu sahihi ila hatujali hivyo vitu sahihi tumevifanya kwa usahihi au lah. Maeneo ya kazi utapewa kazi ya vitu ambavyo ukivitazama si sahihi ila umeambiwa ufanye, ukipata nafasi unaweza kuuliza mbona kinachofanyika hakieleweki? Lakini utaambiwa fanya kwasababu kinatakiwa kufanyika tu.
Hii haimaanishi kwamba hata kama kitu si sahihi hutakikiwi kukifanya kwa usahihi wake? Lah hasha, unatakiwa kukifanya vizuri na kwa usahihi ingawa kimekosewa au hakileti mantiki yoyote kwako na hata kwa kampuni au shilika unalofanya kazi.
Kwani matokeo yoyote yale yatakayotokana na ripoti ya kazi hiyo watakapogundua si kitu sahihi lakini kimefanyika kwa usahihi wake haitakuathiri wewe bali yule aliyeagiza wewe ukifanye. Inamaanisha fuata kanuni na taratibu za msingi na za kisheria zitakazokusaidia endapo chochote kitatokea baadaye.

Usipende kujibizana kwa maneno tu bali kwa ushahidi wa kimaandishi pale unapopewa kazi ya kufanya, unaweza kutumia barua pepe kwamba umepokea hiyo kazi na kama ina matatizo inakupasa uielezee kwenye maandishi na sio maneno matupu unapoenda kuonana na bosi wako. Kwani huwezi kujua ulipokuwa unazungumza naye alikuwa anawaza nini na kama alikuelewa ulichokisema. Lakini katika mambo hayo yote unatakiwa ufanye kwa usahihi wake bila kupindisha pindisha mambo.
Inawezekana unaendelea kujiuliza vitu sahihi ni vipi? Kuna mwandishi mmoja alisema ya kuwa vitu sahihi ni yale maMbo unayofanya kwa juhudi zote kuhakikisha yanakwenda na kufanyika vizuri na kuacha matokeo yatokee yanavyoweza kutokea. Waswahili hupenda msemo unaitwa potelea mbali! Umeagizwa kufanya hivi wewe unafanya vile ambavyo unaona ni sahihi bila kujali matokeo ya maamuzi hayo yatakuwa ni nini? Unahitaji kutambua matokeo ya kila unachokifanya ila tu fanya kwa usahihi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>