Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UPDATES: MOTO WAWAKA BUNGENI, KAGASHEKI AJIONDOA, NCHIMBI, NAHODHA NA MATHAYO WAENGULIWA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi  Kagasheki amejiuzulu wadhifa wake baada ya mjadala mkali wa Bungeni mjini Dodoma.
Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini. Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa, kuchomewa nyumba, mifugo kuuawa, kupigwa na uporaji.
Operesheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo wawajibike.
 
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo David, akitoa utetezi wake, akidai kuwa ameonewa.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBODYA HAPA CHINI

 
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki zichukuliwe. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa amekutaja kuwa ni  muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni busara ushauri wa wabunge utekelezwe.  “Niliona nimtafute mkuu wa nchi (Rais Kikwete), nilimpa picha yote ya kinachoendelea, alikubali ushauri wa Bunge. Amekubali kuchukua uamuzi wa kutengua uteuzi wao (mawaziri).” 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe  James Lembeli (pichani juu) amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa  Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.
Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu  waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.
Akihitimisha mjadala huo wa ripoti ya kamati yake, Lembeli alisema: “...Katibu Mkuu na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii nao wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao na unyama uliotokea kwenye mpango wa Operesheni Tokomeza Ujangili. Rushwa iliyopo ndani ya wizara hiyo ni kubwa inakusanywa kwa kutumia simu, hivyo Serikali izichunguze simu zao kuanzia leo.” 


 

Juu ni Dkt Emmanuel Nchimbi na chini ni Mhe Shamsa Vuai Nahodha 
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>