Sengi
Ilikuwa hadi mwaka 2005 pale wanasayansi walipogundua mnyama aitwaye Sengi (wa familia ya ‘elephant shrew’ anayepatikana Tanzania peke yake
Mara ya kwanza baada ya kupatikana kwenye camera, mnyama huyo alipewa jina ‘Rhynchocyon udzungwensis’ na mtaalam wa mazingira aitwaye, Francesco Rovero. Mnyama huyo mwenye sura ya rangi ya kijivu aitwaye Sengi kwa Kiswahili anapatikana kwenye milima ya huko Udzungwa pamoja na hifadhi ya Kilombero.
Wakipatikana Afrika pekee, wanyama hao wadogo wenye pua kubwa huwafanya wafanane na tembo. Sengi ndio mnyama wa aina hiyo mkubwa zaidi wa aina ya elephant shrews mwenye uzito wa kilogram 0.8 kilogram, ikiwa ni asilimia 25 zaidi ya wengine.
Bado kuna uelewa mdogo kuhusiana na wanyama hao na wanasayansi wanajifunza zaidi. Inasemekana kuwa hujamiana na mnyama mwenzao mmoja tu (monogamous).
CHANZO: NATIONAL GEOGRAPHIC