Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU WAGANGA WA JADI WANAOPIGA RAMLI

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu maalumu ya kutembelea maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino nchini ambapo timu hiyo inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa kuanza na mikoa sugu ya matukio hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora na Shinyanga na baadaye itafuata mikoa mingine. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Picha na Emmanuel Massaka

Na Chalila Kibuda

Serikali imewapiga marufuku waganga wa jadi wanaotumia ramli kutokana na kuwa chanzo cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Mambo Ndani ,Mathias Chikawe wakati alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam,Chikawe amesema waganga wa jadi wanaotumia ramli wamekuwa wakiwaambia watu kuwa kuua au kupata kiungo cha albino ni utajiri,kuwa mvuvi wa mwenye mafanikio.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Chikawe amesema Jeshi la Polisi na Chama Cha Wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) wameunda timu maalum ya kufanya operesheni kwa waganga hao katika mikoa mitatu ikiwa lengo ni kutokomeza mauji ya albino.

“Tunataka kutokomeza mauaji ya Albino kwa timu hii ambayo tumeiunda itapita kila sehemu na wale wote ambao watabainika watachukuliwa hatua na kesi hizo zitapewa kipaumbele na Mwendesha Mashitaka Nchini (DPP)”alisema Chikawe.

Operesheni hiyo ya kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) itafanyika katika Mikoa mitano ambayo inaonekana ni sugu katika matukio hayo, nayo ni Mwanza,Tabora,Simiyu,Shinyanga pamoja na Geita.

Aidha alisema kuhusu serikali kutoamini ushirikina wa kazi hiyo pia itafanywa pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Mikoa na Tawala za Mitaa (Tamisemi) ambapo sheria ya  kuwabana itakapopatikana.

CHANZO: MICHUZI BLOG

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>