Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Viongozi wa Umoja wa wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji pamoja na RPC Dodoma wakiwa katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP akiongea jambo kwenye mkutano wa viongozi wa serikali za mitaa na vijiji uliofanyika katika ukumbi wa Polisi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Afisa Tarafa Dodoma Mjini Bw. HEMEDI SEBASTIAN akiongea na viongozi wa serikali za mitaa na vijiji katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Polisi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP
Mwenyekiti wa Umoja huo Bw. MATWIGA KYATA akiongea katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Polisi.
Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji manispaa ya Dodoma wakisikiliza maelekezo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Polisi
Viongozi wa serikali za mitaa na vijiji wakisikiliza jambo katika mkutano huo.
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amewataka wenyekiti wa serikali za mitaa na vijiji Manispaa ya Dodoma kutekeleza wajibu wao kwa miaka mitano ijayo kulingana na mamlaka waliyopewa na watu waliowachagua kwa kuwa ni watu ambo wapo karibu sana na wananchi ili kuleta amani na utulivu pamoja na maendeleo ya kweli ya kiuchumi, kijamii na kisaiasa.
Kamanda MISIME amesema hayo kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa umoja wa viongozi wa serikali za mitaa na vijiji katika Manispaa ya Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Polisi tarehe 10/01/2015.
Aidha amewaambia viongozi hao kuwa wamepewa uongozi katika kipindi muhimu sana kwani ni kipindi uandikishwaji wa wananchi katika daftari la wapigakura pamoja na kupigia kura katiba pendekezi hivyo wanapaswa kujipanga vizuri kwenye maeneo yao kuhakikisha kunakua na amani, usalama na utulivu.
Nae mwenyekiti wa umoja wa viongozi wa serikali za mitaa na vijiji Bw. MATWIGA KYATA aliyechaguliwa kwa awamu nyingine amesema watatekeleza maelekezo yote ambayo yameelekezwa na serikali kwa mujibu wa sheria ili kuleta amani, usalama na utulivi kwenye mitaa yetu na kufikia maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Vilevile Afisa Tarafa wa Dodoma mjini Bw. HEMEDI H. SEBASTIAN amesema viongozi wanapaswa kufuata miiko iliyopo bila kupendelea mtu yeyote na kutekeleza mjukumu yaliyopo ili kuepusha migongano na migogoro midogomidogo pia tunapaswa kufanya vikao vya mara kwa mara ili kukumbushana mambo mbalimbali yatakayotufanya tufanikishe katika uongozi wetu.