Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Tabia ya baadhi ya wajawazito mkoani shinyanga kutokuona umuhimu wa kuhudhuria kwenye vituo vya afya na kliniki imesababisha wanawake 64 kupoteza maisha katika kipindi cha mwaka 2014 kutokana na kujifungulia nyumbani na kukosa huduma muhimu pale walipopata matatizo wakati wa kujifungua.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Ntuli Kapologwe, ameiambia Radio One Stereo kuwa kutokana na utafiti walioufanya wamebainisha kuwa asilimia hamsini ya akina mama wajawazito mkoani humo, hujifungulia kwa wakunga wa jadi, hali ambayo imekuwa ikichangia kuongezeka kwa idadi ya vifo vitokananvyo na uzazi.
Amesema vifo vingi kwa akina mama hao vinachangiwa na mila na desturi na kuwa wanawake wanao pata ujauzito wakiwa na umri mkubwa wamekuwa wakiona aibu kwenda vituo vya afya na kwenye hospitali kuzalishwa na wauguzi wenye umri mdogo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBONYEZA HAPA CHINI
Dkt. Kapologwe amesema kutokana hali hiyo tayari wameanza kutoa elimu kwa akina mama hao, kujua umuhimu wa kujifungulia hospitalini, zahanati au vituo vya afya huku akiwataka kuwaamini wauguzi wenye umri mdogo kuwa kazi wanayoifanya ni ya kitaaluma kama wanavyofanya wakubwa na hivyo wasiwaonee aibu wala kuwadharau.
Kwa upande wao baadhi ya wanawake wa mjini Shinyanga wakiwemo Elizabeth John na Liliani Mwese, wamesema asilimia kubwa ya akina mama hawapendi kuzalia hospitali, zahanati na vituo vya afya kwa kuwa baada ya kujifungua wauguzi huchukua kondo la nyuma na kulitupa badala ya kulifukia ardhini kama mila na desturi za kwao zinavyoelekeza.
Wamesema kutupa kondo la nyuma kwa maelekezo ya mila na desturi zao ni sawa na kumtupa mtoto na kuwa wanaamini kwamba pamoja mambo mengine ni kukaribisha mikosi ya kutojifungua salama kwenye familia.
CHANZO:ITV TANZANIA