Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Afisa Miradi wa ForumCC Fazal Issa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
Mwezeshaji kutoka Youth Can Tanzania, Rahma Mwita, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
Afisa Miradi huyo amesema katika mkutano huo wa Peru kulikuwa na makundi mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia yakiwamo kundi la nchi za Afrika ambazo ndizo zimekuwa muathirika mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi. Mkutano huo pia ulizikutanisha nchi 72 zilizokwenye kundi la nchi zilizoendele na ambazo ni chanzo kikuu cha uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa na viwanda vinavyozalisha hewa ukaa na kuongeza joto duniani.
Aidha Afisa huyo amesema kuwa kulikuwa na kundi kutoka nchi za Bara la Asia na kundi la nchi za visiwa pamoja na makundi mengine ya wanaharakati wa mazingira ambao walipigana kuzibana nchi zilizoendelea kupunguza uharibifu na kutoa pesa kwa nchi zilizoathirika na zinazoendelea kuathirika na mabadiliko ya tabianchi.
Amesema nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania walikuwa na msimamo mmoja ambao ni kupunguza gesi joto duniani , na kuzitaka nchi zenye viwanda kutoa fedha zaidi katika mfuko wa pamoja wa mazingira katika kujenga uwezo kwa nchi maskini na zinazoathirika kupunguza na kumaliza changamoto za mabadiliko ya tabianchi
“Zinahitajika dolla bilioni 100 kwa mwaka katika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi duniani na kiasi kilichochangwa ni dolla bilioni 10 sawa na asilimia 10% tu ya fedha ambazo zinazohitajika, Utaona hapo ni kwa kiasi gani nchi zilizoendelea zinahitajika kuchangia mfuko huu” anasema Fazal.
Afisa Habari ForumCC, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya mrejesho wa yaliyojiri kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi COP20 uliofanyika Peru mwishoni wa mwaka jana.
Naye katibu mkuu wa asasi ya kiraia ya (Youth-CAN) Justine Mponda amesema wao kama vijana wapambanaji wa mazingira hapa nchini wameshiriki katika mkutano huo wa COP 20 Peru kwa lengo la kujifunza zaidi kutoka kwa vijana wenzao duniani walioshiriki katika mkutano huo wa mabadiliko ya tabianchi.
“ tunajihusisha na kutoa elimu ya mabadiliko ya tabianchi kwa jamii juu ya athari ya mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na kuwashawishi vijana nchi juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Pia kufikisha madai na vilio vya vijana nchini waathirika wa mabadiliko ya tabia nchi kwa serikali na taasisi za kimataifa kwa utatuzi zaidi”
Taasisi hiyo ya Youth –CAN ina lengo la kufanya kampeni nchini kabla ya mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa mwaka huu Paris Ufaransa. Kmpeni yenye lengo la kuwafikia watu zaidi ya milioni 1 nchini ambao ni makundi ya vijana, wazee, wanawake na wanahabari na katika kampeni hiyo watatumia usafiri wa baiskeli katika ile hali ya kuepuka kuchafua mazingira.
Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi maarufu kama COP20 ulifanyika jijini Lima nchini Peru kuanzia Desemba mosi na kumalizika Desemba 14 mwaka 2014 ambao ulikuwa na malengo ya kujadiliana na kupitisha maadhimio ya mkataba ambao utaenda kusainiwa mwishoni mwa mwaka huu jijini Paris Ufaransa