Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WENYEVITI NA WAJUMBE WA SERIKALI ZA MITAA WILAYA ILALA WAAPISHWA LEO

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Baadhi ya Wajumbe wa Serikali za Mitaa waliopatikana katika Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea wakila kiapo mbele Wakili wa Serikali kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
 Baadhi ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliopatikana katika Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea wakila kiapo mbele Wakili wa Serikali (hayupo pichani) kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
 Sehemu ya Wenyeviti na Wajumbe wao wakiwa nje ya Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo wakisubiria kuitwa majini yao kwa ajili ya kwenda kula viapo.
 Sehemu ya Wenyeviti na Wajumbe wao wakijaza fomu za viapo kabla ya kuapishwa.

Na Chalila Kibuda 

Wenyeviti wa  Serikali ya Mtaa wa wa Kwalala na  Kigogo Fresh B  wa Chama cha Mapinduzi (CCM)waameshindwa kuapa kuwa mwenyekiti wa  kutokana na kudaiwa sio wa washindi katika nafasi hiyo.

Zuio la kushindwa kuapishwa kwa viongozi hao kulizua mgogoro kati ya chama cha CCM  na Chadema na  kulazimika Jeshi la Polisi kuwaondoa viongozi hao.

Wenyeviti hao ni  Mariano Maurus CCM  na Patriacian Mamakula Chadema ,kila mmoja anadai ndiye mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigogo Fresh B.

Katika  Mtaa wa Kwalala wagombea ni Doricasy Lukiko wa Chadema na Khadija Sidemoga wa CCM wote wanadai kuwa wameshinda uchaguzi wa serikali ya Mtaa huo katika nafasi ya Mwenyekiti.

Mariano Maurusy alisema yeye ndiye mshindi wa Mtaa wa Kigogo Fresh alimshinda Patrician Mamakula wa Chadema ,kuwa CCM ilipata kura 233 na Chadema kura 228.

Alisema kuwa wanachama wa Chadema walifanya vurugu katika uchaguzi huo kwa kuchoma kura bila kujua msaidizi wa uchaguzi alikuwa na nakala zinazoonyesha ushindi wa mwenyekiti na wajumbe wa CCM.

Wanachama wa Chadema walidai kuwa anayejiita mshindi kwa tiketi ya CCM ni muongo wanapoteza ukweli juu ya uchaguzi huo kwa kuaminisha wameshinda kumbe sivyo.

CHANZO: MICHUZI BLOG


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>