Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Vijana watatu kutoka nzega wametembea kwa miguu kwa siku 37 hadi jijini dar es saalam kwa lengo la kutaka kwenda kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha malamiko yao ikiwenmo kukithiri kwa vitendo vya rushwa na ubadilifu wa rasilimali za umma lakini safari ya vijana hao ikaishia mikononi mwa polisi baada ya kukadi agizo halali la mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh. Jordan Rugimbana la kuwataka wafuate taratibu za kumuona kiongozi huyo wa nchi.
Vijana hao ambao walivamia magunia na kusema kuwa wamevaa hivyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha uchungu wa namna ambavyo rasilimali za taifa zisivyowanufaisha wazawa.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia matembezi hayo wamewataja vijana hao kama ni wazalendo ambao ujumbe wao unawagusa mamilioni ya watanzania ambo hawana ujasiri na uwezo wa kufanya kitendo cha kijasiri kama hicho.
Baada ya vijana hao kufika kwa mkuu wa wilaya walifanya mazungumzo naye ambapo mkuu huyo aliwataka wafuate taratibu za kumuona rais na kusisitiza kuwa matembezi hayo yalipaswa kuishia hapo.
Kufuatia maagizo hayo vijana hao hawakukubaliana na agizo hilo na kusema wao bado ni yao ya kwenda ikulu Ipo pale pale na ndipo walipioanza safari nyingine kuelekea huko na kabla ya hapo walitoa matamko yao mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya kablya ya kukamtwa na kupelekwa kituo cha polisi magomeni.
STORI NA ITV TANZANIA