Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwanamme mmoja raia wa Uturuki aliyempiga risasi na nusura amuue aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki papa John Paul wa pili mwaka 1981 ameweka maua kwenye kaburi lake katika makao makuu ya kanisa katoliki ya Vatican. Ziara ya Mehmet Ali Agca kwenye makao ya Vatican inafanyika miaka 30 tangu John Paul amtembelee gerezani na kumsamehe kwa kujaribu kumuua.
Bwana Agca aliomba kukutana na kiongozi wa sasa wa kanisa katoliki papa Francis lakini hata hivyo ombi lake lilikataliwa Aliachiliwa kutoka gerezani nchini Italia mwaka 2000 na kisha baadaye akatumikia kifungo chengine cha miaka 10 nchini Uturuki kwa makosa tofauti. Hadi sasa sababu zake za kutaka kumuua papa John Paul hazijulikani.
CHANZO: BBC SWAHILI
CHANZO: BBC SWAHILI