Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

PICHA: TAARIFA ZA MWANZO KUHUSU NDEGE YA AIRASIA QZ8501 YAPOTEA IKIWA NA WATU 162 LEO ASUBUHI

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Ndugu, jamaa na marafiki wa abiria waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia QZ8501 wakiwa na majonzi wakati wakisubiri taarifa kuhusu ndugu zao katika Uwanja wa Ndege wa Surabaya, Indonesia.
 Ndege ya AirAsia, QZ8501 iliyokuwa na watu 162 ikitokea Indonesia kwenda Singapore imepoteza mawasiliano leo asubuhi.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Kati ya watu hao 162, abiria walikuwa 155, marubani 2 na wafanyakazi wa ndege hiyo 5. Watu 157 ni raia wa Indonesia, 3 raia wa Korea Kusini, 1 kutoka Malaysia na 1 raia wa Singapore.
 Imeelezwa kuwa kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano, rubani aliomba kubadili uelekeo wa kawaida kutokana na hali mbaya ya hewa. Ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo kwa mara ya mwisho Novemba 16, 2014 kama ilivyokuwa imepangwa.
 Rubani wa ndege hiyo ana uzoefu wa saa 6,100 angani huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 2,275.
 Miongoni mwa abiria 155 waliokuwa kwenye ndege hiyo, 138 ni watu wazima, 16 watoto na 1 mama mjamzito.
QZ8501 imetoka Indonesia saa 11: 27 alfajiri na ilitarajiwa kuwasili Singapore saa 2:37 asubuhi.
 Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>