Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WAFANYAKAZI KUGOMEA UCHAGUZI 2015 KAMA WASIPOLIPWA BILIONI17 ZA MADAI YAO

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Katibu mkuu wa Shirikisho la wafanyakazi [TUKTA] Nicholous Mgaya akifafanua jambo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa serikali za mitaa [TALGWU] unaofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma.
 Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Serikali za mitaa TALGWU wakifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo mjini Dodoma.

Katibu mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUKTA Nicholous Mgaya na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa TALGWU Suleman Kikingo wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa Baraza hilo mjini Dodoma.

NA JOHN BANDA, DODOMA
KATIBU mkuu wa chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mtaa [ TALGWU] Suddy Madega amesema iwapo serikali haitawalipa wafanyakazi fedha zao jumla ya Bilion 17 chama hicho kitasusia uchaguzi mkuu ujao.
Katibu huyo ameitoa kauri hiyo  mjini Dodoma kwenye mkutano wa baraza kuu la TALGWU  unaofanyika katika ukumbi wa Loyal Village kwa siku tatu.
Katibu mkuu huyo amesema Baraza hilo limekutana likiwa na agenda kubwa za mkokotoo, Mifuko ya hifadhi na madai ya msingi ya wafanyakazi kwa serikali, ambapo kuhusiana na swala la madai hayo ya wafanyakazi
watakabana vilivyo na serikali. Madega amesema watawambia wanachama wao wagome katika uchaguzi mkuu ujao iwapo serikali haitatekeleza makubaliano kati yao ya kuwalipa madai ya wafanyakazi 17. Bil  mpaka uchaguzi utakapofika.
Ameongeza kuwa TALGWU ina wanachama kila mahali ikiwemo vijijini hivyo watawambia wasijihusishe na upigaji kura huo, kwa sababu hawawezi kuendelea kuchagua viongozi wasiowajali wafanyakazi. Aidha kwa upande wake Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi [TUKTA] Nicholaus Mgaya amesema Watakutana na Rais Kumwambia kuhusu kutolipwa mpaka hivi sasa wakati tayali Waziri mhusika alishaahidi kulipa Deni hilo na kinachowashtua ni kutolipwa mpaka leo ambapo kama wasipofanya hivyo mgomo wa ktoshiriki uchaguzi
ujao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>