Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

WAKURUGENZI WATANO WASIMAMISHWA KAZI KWAKUSHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAO WA KUSIMAMIA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema leo Jumatano Desemba 17, 2014, kuwa hatajiuzulu ng’o kutoka wadhifa wake, kufuatia kashfa ya kuvurugika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini Jumapili iliyopita.
Waziri Ghasia, akitoka kwenye chumba cha mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Waziri Ghasia na katibu mkuu wa TAMISEMI, Jumanne Sagini

Serikali imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita wa Halmashauri, na kuwasimamisha kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana na kubainika kuchangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, mwezi huu.
Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema uamuzi huo pia umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Mhe. Ghasia amewataja wakurugenzi hao waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni 

1.      Bwaba Benjamin A. Majoyo ambaye ni mkurugenzi  Mtendaji wa halmashauri ya Mkuranga,
2.      Bwana Abdalla NgoduMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliuwa,
3.      Bwana Masalu MayayaMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kasulu,
4.      Bibi Goody PambaMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Serengeti,
5.      Bwana  Juliusi A. MadigaMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema na
6.      Bwana Simon C. R. Mayeye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bunda

Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni-:

i)                    Bw.Felix T.Mabula, Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya  Hanang’
ii)                   Bw.Fortunatus Fwema, Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya  Mbulu
iii)                 Bi.Isabela D.Chilumba, Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya   Ulanga
iv)                 Bi.Pendo Malabeja, Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya  Kwimba
v)                  Bw.William Z. Shimweta, Mkurugenzi  Mtendaji wa  Manispaa ya  Sumbawanga 

 Waziri Ghasia amesema kuwa Wakurugenzi wengine watatu wapewa onyo kali, ambao ni w

i)                    Bw.Mohamed  A.MajeMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rombo
ii)                   Bw.Hamis YunaMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Busege
iii)                 Bw.Jovin A.JunguMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muheza


 Na pia wakurugenzi walopewa onyo ya kawaida ni
i)                    Bw.Isaya Mngulumi Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilala 
ii)                   Bw.Melchizedeck HumbeMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya  Hai
iii)                 Bw. Wallace J. KariaMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya  Muheza

Na Pamoja Blog


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles