Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Watanzania waendelea kufaidika kutoka kwa hospitali ya Apollo iliyoko nchini India. Hii ni kufuatia hosiptali hiyo kufanikiwa kuwatenganisha mapacha wa kike Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na tumboni kutoka nchini Tanzania katika upasuaji uliofanyika tarehe 17 Novemba 2014 nchini India. Mapacha waliounganika kwa mtindo huu hujulikana kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.
Mapacha Abriana na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya kifua na tumbo, hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo na maini yaliyounganika. Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa kwa madaktari ulikuwa kufanya utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi ambayo waliweza kukabiliana nayo ipasavyo kutokana na madaktari waliokuwepo wenye wataalum wa kiufundi na matibabu.
Upasuaji huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbali mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa masaa 11. Watalaamu walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyo kuwa vimeungana lakini mapacha hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo kusaidia zoezi zima la uponyaji baada ya upasuaji.
Hali kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa kurudisha viungi husika katika mahala pake baada ya kuvitenganisha. Akizungumzia kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive Surgeon anasema, “Baada ya upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa nne kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahala pake.”
Upasuaji huu wa mafanikio wa mapacha waliounganika kutoka ncini Tanzania sio wa kwanza kufanywa na hospitali ya Apollo. Mwishoni mwa mwaka 2013 mapacha wengine wakiume waliokuwa wameungana na kujulikana na wataalamu kama Pygopagus, Ericana & Eluidi kutoka Tanzania walifanikiwa kutenganishwa na wataalamu wa hospitali hiyo. Matukio amabayo yamepandisha chati na kuipa hadhi ya juu hospitali ya Apollo iliyoko nchini India na nchi ya India kwa ujumla kama kiongozi katika sekta ya afya na mfano wa kuigwa na nchi nyingine ikiwemo Tanzania. Hospitali hiyo ina mahusiano mazuri na nchi ya Tanzania ikitembelewa idadi kubwa ya wagonjwa kutoka Tanzania kutokana na ukosefu wa huduma muhimu na za kisasa nchini.
Wapacha walioungana hutambuliwa na kupewa majina kutokana na jinsi muungano huo unapokuwa katika viungo mbali mbali vya mwili. Ikiwa aina ya mapacha waliounganika wa Thoraco Omphalopagus ndio inayoongoza kuripotiwa kwa asilimia 28% zaidi ya aina nyingine zote zinazotambulika matukio mengi yakitokea zaidi Kusini-Magharibi mwa bara la Asia, Africa and Brazili. Katika aina hii mapacha wanakuwa wameunganika kuaznia kifuani mpaka chini ya kifua kwenda kwenye tumbo na hutumia baadhi ya sehemu ya moyo, ini na baadhi ya sehemu viungo vya mmeng’enyo wa chakula(i).
Kulingana na hospitali ya Apollo kesi zinazohusu mapacha waliounganika huwa ni nadra mathalan moja kati ya uzao 200,000 huonekana. Lakini, asilimia 60 ya hao hufariki wakati asilimia 35 hufariki katika kipindi kifupi baada ya kuzaliwa kutokana na sababu mbali mbali (ii).
Akizungumzia upasuaji huo uliokuwa na mafanikio, Dkt. Prathap C Reddy, Mwenyekiti na Muanzilishi wa Hospitali za Apollo anasema, “Nikitazama katika mwaka huu wa 2014 naona maisha ya watu tuliweza kuyagusa kwa namna njema. Mbali na maumivu wanayopata watoto yatokanayo na ugonjwa, wazazi pia hupitia mshituko na mahangaiko makubwa. Nchi nyingi za bara la Afrika zinakosa tiba muhimu na mbadala na hivyo kujikuta wanakuja nchini India kupata huduma hizo muhimu na kisasa. Inafurahisha na kuleta faraja kuwa katika sikukuu hii ya Krismasi Jimmy na Carolyn watarudi nyumbani na watoto wao wakiwa ni binadamu wawili tofauti.”
Tangu mwaka 2007, jozi nane za mapacha waliounganika katika ini na utumbo kutoka sehemu mbali mbali nchini India zimeripotiwa kutenganishwa. Aradhana na Stuthi ni jozi pekee ya mapacha waliwahi kutenganishwa kwa upasuaji wakiwa na mioyo iliyo katika mvungu (cavity) mmoja hali sawa na mapacha Adrianan na Abriana. Japo moja ya mapacha wa thoraco opmhalopagus Aradhana kufariki wiki tatu baadae, Adriana and Abriana na ndio aina hiyo ya mapacha walioweza kuishi baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa.
Baada ya miezi ya matibabu, mapacha Adriana na Abriana kutoka Dar-es-Salaam watarejea nyumbani Tanzania tarehe 18 Disemba na kufika mjini Dar es Saaam asubuhi ya tarehe 19 Disemba. Katika kipindi hiki cha sikukuu itakuwa shangwe kwa wazazi Jimmy na Carolyn wanaporudi nyumbani kutoka nchini India wakiwa na watoto wao wawili waliotenganishwa.