Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Namna gani unachagua shahada ya kwenda kusoma? Miaka ya hivi karibu watu wameendelea kupata shahada za kutosha kabisa na huku vyuo vingine vikikuhakikishia kupata kazi baada tu ya kumaliza masomo kwenye vyuo vyao. Lakini je tunachaguaje shahada hizo? Unahitaji kujua kitu gani unakwenda kusomea kabla ya kwanza kusoma , ingawa mawazo haya yanaweza kuwa kama hayawezekani kwani watu wengi wanadhani unatakiwa kubahatisha mengine utarekebisha mbele kwa mbele.
Hi ni karne yenye ushindani mkubwa hivyo hata habari ya kubahatisha inakubidi uachane nayo kidogo na kutumia akili ya ziada. Inatubidi tufungue macho na kuwafundisha wadogo zetu hali halisi na maisha yanakokwenda bila kupindisha maneno,
Vitu vya msingi vya kuangalia ni kwamba si rahisi kwa sasa kwamba ukimaliza shahada utapata kazi kirahisi hivyo unahitaji kuweka juhudi kubwa katika masomo yako na kazi kwa vitendo zaidi kuliko kuangalizia au chabo kwa lugha ya shule shule.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Tatizo lililopo sasa si shahada bali watu wenye ujuzi wa kile walichosomea ni wachache sana wengi wanabahatisha au hawajui wanachopaswa kufanya. Kwanini wanafanya hivyo, ni kwa sababu ya mfumo wetu wa elimu ambao unategemea kufanya mitihani mingi zaidi kuliko kumpa mwanafunzi ujunzi wa kumsaidia. Usishangae kuone mtu mwenye shahada ya elimu ya juu ya chuo kikuu maisha yanamshinda huku elimu anayo, unajiuliza tatizo kwani ni nini?
Kwanza unasoma au unakwenda kujiunga na chuo gani na je kinakidhi mahitaji unayoyataka?
Hi kama wewe mwenyewe unajua unataka nini tofauti na kile unachoshauliwa kwenda kusoma na wazazi au marafiki na mara nyingine kwa kufuata mkumbo. Unahitaji kujua unahitaji elimu ya nini na ikusaidie kwenye kitu gani lasivyo utaishia kufanya kitu ambacho haukukihitaji sana ila umekifanya na unaona hakikusaidii.
Unatakiwa kuchagua kitu ambacho kitakusaidia kama utapata kazi au usipopata kazi bado utaweza kuishi kwa elimu hiyo. Usifanye maamuzi ambayo yatakufunga au kukufanya kuwa mtumwa wa kisasa kimazingira na kiufahamu.
Elimu uliyonayo inatakiwa kukukomboa na sio kukufanya mtumwa tena, hivyo kwanini unakwenda shule ? Kitu gani kimekosekana kwako na unahitaji kuongeza ufahamu wako au unahitaji kuongeza cheti? Ufahamu na cheti ni vitu viwili tofauti, kuna watu wanafukuzia vyeti na kusahau kuongeza ufahamu wao wa kiutendaji na kuonyesha matokeo bora zaidi hivyo wanashangaa kwanini hawaogezewi mishahara au kupandishwa vyeo. Kiwango chako cha elimu kinatakiwa kiendane na matokeo unayotoa kiutendaji katika kazi au maisha yako binafsi, tofauti na hapo tunadanganyana.