Lupita
Mtandao wa Yahoo umetoa orodha yake ya filamu 25 bora zaidi mwaka 2013. Katika orodha hiyo, nafasi ya kwanza imekamatwa, na ’12 Years a Slave’ filamu ya utumwa ambayo pamoja na waigizaji wengine, Mkenya Lupita Nyong’o ameigiza pia.
Lupita kama Patsey
Ni filamu iliyotokana na kitabu cha mwaka 1853 cha Solomon Northup, mtu mweusi aliyezaliwa New York lakini akatekwa mjini Washington, D.C. mwaka 1841 na kuuzwa kama mtumwa.
Filamu hiyo imeongozwa na Steve McQueen na kuandikwa na John Ridley. Muigizaji Chiwetel Ejiofor ndiye aliyecheza kama Solomon Northup na amejichukulia sifa nyingi kwa uhusiaka huo.
Lupita ameigiza pia kama mtumwa aitwaye Patsey.