Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

PICHA : ZIARA YA CHADEMA BUNGE LA ULAYA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Jumbe Safari akiwa na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, walipokutana jana mjini Brussels, Ubelgiji kwa mazungumzo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya ujumbe wa CHADEMA kufuatia mwaliko wa bunge hilo
 Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Patrobas Katambi. Ujumbe wa CHADEMA ukiongozwa na mwanadiplomasia mahiri Profesa Abdalla Safari, uko nchini Ubelgiji kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Safari Abdalla akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP) Rainer Wieland wakati ujumbe wa CHADEMA ulioko nchini Ubelgiji, ulipofika ofisi za bunge hilo mjini Brussels kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa BAWACHA, Grace Tendega na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri John Mrema.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demoikrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Safari na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, wakati ujumbe wa CHADEMA ulipofika Ofisi za EP kuanza ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>