Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja mkazi wa kijiji cha kindo wilaya ya mvomero mkoani morogoro amekufa baada ya kunyongwa na baba yake wa kambo kufuatia migogoro ya kifamilia kati yake na mkewe.
Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Leonard Paul amesema mtoto Abdalla Hamis amenyongwa na baba yake wa kambo Zamili Shabani (27) muda mfupi baada ya mamawa mtoto kwenda dukani kununua mahitaji na aliporejea aliingia chumbani kumwamsha mtoto ndipo akagundua kuwa mtoto amekufa ambapo muhumiwa kwa wasiwasi alianza kukimbia na mama huyo alipiga kelele ya kuomba msaada kwa majirani hadi alipokamatwa.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoa wa morogoro linamshikilia mtuhumiwa mmoja Abadalla Kifungo (40) mkazi wa malola wilaya ya ulanga mkoani morogoro kwa tuhuma kukutwa na slaha aina ya shortgun na risasi mbili ambapo inasadikiw anatuhumiwa alikuw aakijihusisha na matukio ya ujangili ambapo watuhumiwa hao wa matukio mawili tofauti watafikishwa mahakamani kujibu Mashtaka.
CHANZO: ITV TANZANIA