Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TAMBUA SABABU SABA(7) ZA KWANINI HUTAKIWI KULA LUNCH KWENYE MEZA YAKO YA KAZI

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Inawezekana unahitaji ushawishi mkubwa wa kwanini unatakiwa kwenda kula chakula cha mchana nje ya ofisi au mbali na meza yako ya kazi. Hapa kuna sababu za kukutosha uelewe kwanini unatakiwa kufanya hivyo;


1. Morali yako ya kazi inaongezeka
Wewe sio mashine kama binadamu wa kawaida kuna vitu fulani hula unafikia kikomo kwenye mwili wako kama unapenda kukubaliana au la! Ili uweze kufanya kazi vizuri unahitaji kutoka nje ya meza yako mara kasha kwa siku na hii ni pamoja na kwenda kula cha kula cha mchana bali na meza yako ya kazi.

2. Utaongeza ubunifu katika utendaji wako wa kazi
Kama nilivyoweza kuongelea kwenye pointi ya kwanza kwamba unaongeza morali wa kazi . Je ulishawahi kukutana na hali ya kufikiria zaidi au kupata mawazo mapya ukiwa bafuni kuoga au ukiwa unatembeatembea? Je wewe unadhani linakutokea hilo peke yako? Hii inampata karibu kila mtu. Unapoupa mwili au akili yako nafasi ya kuwa huru kwa muda fulani. Ubongo wako unapata fursa ya kuwaza vitu vipya na kukusaidia hata kujibu maswali ambayo yalikuwa magumu ulipokuwa kwenye dawati lake la kazi. Hivyo unashauriwa kuyapa mawazo yako muda wa kupumzika wakati wa chakula cha mchana ili kuruhusu uwezo wa akili kuendelea kufanya kazi vizuri.

ENDELEA KUSOMA MAKALAHII KWAKUBOFYA HAPA CHINI

3. Unapokwenda nje au kula na watu wengine inakusaidia kuboresha mahusiano yako na wafanyakazi wenzako
Kama wewe hupendelea kwenda kula mara chacha chache sana, utakuta hata mahusiano yako na watu wengine kazini yanakuwa kama yanasua sua. Kumbuka uhusiano wako na watu wengine ofisini ni wa muhimu sana, kwa kuzingatia ni maisha unayoyaishi kila siku ukiondoa Jumamosi na Jumapili. Hii haimaanishi uwafanye wafanyakazi wenzako marafiki wa kushibana, bali unaboresha uhusiano na kurahisisha utendaji wako wa kazi na watu wengine.

4. Kukaa sana si vizuri kwa afya yako
Mwili wako unahitaji kufunguka au kutembea, wataalamu wa afya wanashauri kwamba unapotumia muda mwingi kukaa kunahatarisha afya yako na hasa unapokaa kwa muda mrefu sehemu moja.

5. Unafurahia chakula chako vizuri zaidi
Kuna watu wanapenda kula huku wakifanya kazi, bali ukitaka kufurahia chakula unachokula unahitaji kutulia kuelekeza mawazo yako huko na hapo ndipo utaweza kufurahia zaidi chakula. Kwanini huwezi kufurahi wakati uko mezani kwako, ni kwasababu utaendelea kufikiria kazi hivyo chakula kushindwa kupanda vizuri.

6. Unaweza kutumia muda wako wa mchana kama muda wa kuongeza mtandao wako wa mawasiliano na watu wengine na vile vile kupata fursa kwenye taaluma uliyopo.
Katika dunia hii kazi ni ya muda tu, hiyo inamaanisha we tayari kukutana na fursa mpya kwani kuwa na mtandao wa mawasiliano ni zaidi ya kupata marafiki wapya. Hii inakusaidia kukutana na watu wanaofanya vitu tofauti na vya kwako hivyo kujifunza kutoka kwao na wao kujifunza kutoka kwako.

7. Unaweza kutumia muda huo kuwasiliana na marafiki wako wa zamani
Kuna wakati tunakuwa na shughuli nyingi kiasi kwamba tunasahau marafiki zetu. Tunahitaji marafiki ili kufurahi na kuwa na maisha ye afya, usijisikie vile unapotakiwa kwenda lunch. Kuna vitu vingi vinavyokusaidia unapotoka na kupumzika badala ya kufanya kazi mfululizo hivyo ni wakati wa wewe kuangalia faida na hasara kwa kila kitu unapofanya kwako na kwa jamii inayokuzunguka.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>