Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Margareth Chacha (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tandika Vicoba Group (Tavico), uliofanyika katika viwanja vya Kanisa Katoliki la Chang'ombe Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tavico, Sarah Chikuni, wengine ni wanachama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Margareth Chacha (kulia), pamoja na Mwenyekiti wa Tavico, Sarah Chikuni wakikata keki maalumu ya uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Kanisa Katoliki la Chang'ombe Dar es Salaam jana
Hapa ni mserebuko kwa kwenda mbele.
Wanachama wa Tandika Vicoba Group (Tavico), pamoja na wageni waalikwa wakiserebuka katika hafla ya uzinduzi wa Tavico uliofanyika viwanja vya Kanisa Katoliki la Chang'ombe Dar es Salaam leo.
Wanachama wa Tavico wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanachama wa vicoba kutoka Yombo Makangarawe nao walijumuika katika uzinduzi huo.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com)
Hapa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Maofisa kutoka Tavico, Mariam Shabani (kushoto) na Mariam Ndunguru ambaye ni mlezi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Tavico, Sara Chikuni akimkaribisha mgeni rasmi, Mama Chacha katika sherehe hiyo.
Ni furaha tupu katika uzinduzi huo.
Ni kuserebuka tu. Chezea uzinduzi wewe mbona raha.
Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), nao walikuwepo. Kutoka kushoto ni Masanyika Choka na Sunday Mziray.
Wanahabari nao walikuwepo kuchukua taarifa hiyo.
Tuserebuke tuserebuke mpaka chini. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com)