Habari iliyoifikia hivi punde toka jijini Arusha, inaeleza kuwa Ndege ya abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha,hali iliyopelekea Ndege hiyo kusimama nje kabisa ya uwanja huo huku abiria zaidi ya 200 wakiwa ndani ya ndege hiyo mpaka sasa bila ya kushuka.
Taili la ndege likiwa limefunikwa na mchanga baada ya kushuka ghafla kwenye uwanja wa ndege wa Arusha
Wataalam wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.
Huu ndio mwonekano wa tairi la mbele la Ndege ya abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) likiwa limekwama kwenye majani na kuchimba mchanga
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wataalam wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.
Huu ndio mwonekano wa tairi la mbele la Ndege ya abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) likiwa limekwama kwenye majani na kuchimba mchanga
Tuinaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo, na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa zitakavyokuwa zinakitufikia.
PICHA NA MDAU WETU KUTOKA ARUSHA
PICHA NA MDAU WETU KUTOKA ARUSHA