Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa Skafu na vijana na wa Chipukizi wakati alipowasili eneo la Somanga wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi akianza ziara yake ya siku 16 katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza sughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi, Katibu Mkuu huyo anaongozana naNape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi na Mbunge jimbo la Mtama Mh. Bernald Membe.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SOMANGA-KILWA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kilwa na Mkoa wa Lindi waliofika katika eneo la Somanga kwa ajili ya mapokezi Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kumpokea katika eneo la Somanga wilayani Kilwa kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kumpokea katika eneo la Somanga wilayani Kilwa kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega wakati akielekea kushiriki ujenzi wa jengo la VICOBA Mwamko Somanga.
Mmoja wa wasanii Ali Said Abubakary akicheza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ukumbi wa VICOBA Mwamko Somanga. Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi na Mbunge jimbo la Mtama Mh. Bernald Membe akizungumza na wananchi katika mji wa Somanga mara baada ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mkuu wa mkoa wa Lindi Magalula Sid Magalula akiwasalimia wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM akinyanyua mkono wake juu kuashiria kupokea salamu zao.
Mkuu wa mkoa wa Lindi Magalula Sid Magalula akiwasalimia wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM akinyanyua mkono wake juu kuashiria kupokea salamu zao.