Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MWANAMKE MJAMZITO WA INDIA APATA ‘MISCARRIAGE’ NA KUPOTEZA WATOTO 10 KWA USIKU MMOJA

$
0
0

Mwanamke aliyekuwa mjamzito wa watoto kumi nchini India ameripotiwa kupata ‘miscarriage’ (kuharibika kwa mimba) na kupoteza watoto wote kumi kwa usiku mmoja wiki hii.

Kwa mujibu wa mtandao wa Indian Express, mwanamke huyo mwenye miaka 28 aitwaye Anju Kushwaha aliyekuwa na ujauzito wa watoto kumi, Jumapili iliyopita alipata ‘miscarriage’ na kupoteza watoto tisa akiwa njiani kuelekea hospitali, na baada ya kufika hospitali masaa mawili baadaye alimpoteza na mtoto wa kumi aliyekuwa amesalia.
Dr Santosh Pathak alisema mwanamke huyo na mume wake waliwasili hospitali kabla ya saa sita usiku, wakiwa wamebebea viumbe tisa (fetus) waliowafunga kwenye kipande cha nguo baada ya mimba kutoka wakiwa njiani.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Dr Randhir Singh, rais wa ‘Madhya Pradesh chapter of Indian Fertility Society’ amesema tukio kama hilo ni nadra sana kutokea kwa India, ambapo linaweza kuwa moja ndani ya milioni.
“I have seen up to five foetuses in one womb but never so many,” alisema Dr Meena Bhargava, HoD wa idara ya gynaecology , na kuongeza kuwa viumbe hivyo vilikuwa na umri wa kati ya miezi miwili au mitatu na nusu.

Source: Indian Express

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>