China imetangaza kupeleka chombo kisichokuwa na binadamu mwezini kilichotua kwa mafanikio kwa mara ya kwanza tangu miaka 37 iliyopita.
Hiyo ni mara ya kwanza China kufanya hivyo na kuifanya kuwa nchi ya tatu duniani baada ya Marekani na USSR. Chombo cha USSR kilitua mwezini mwaka 1976.
Chombo cha China kilichotua mwezini kilipewa jina la Chang’e 3 na kiliondoka duniani December 2 na kutumia siku 12.