Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kituo cha redio cha Times FM na kampuni ya Times Promotions, wamewasilisha mashtaka mahakamani ya kutaka viongozi wa juu wa Clouds FM pamoja na msanii wa Nigeria, Davido wapelekwe jela kwa kukaidi amri ya mahakama.
Kampuni hiyo kupitia wakili wake Peter Kibatala imewasilisha mashtaka hayo katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Jumatatu hii.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Davido na Clouds FM walikaidi amri ya mahakama iliyotolewa kumtaka Davido asitumbuize kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika October 18 kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Times FM walikuwa wameshaingia mkataba na Davido atumbuize November 1 kwenye tamasha lao ambalo linadaiwa kuahirishwa kutokana na kilichotokea.
Soma zaidi habari hiyo iliyoandikwa kwenye gazeti la leo la Daily News hapa.