Jeneza la Mandela likitolewa katika ndege ya kijeshi iliyompeleka nyumbani kijijini Qunu.
Mwili wa hayati Nelson Mandela umepelekwa katika mkoa wa Eastern Cape kwa safari ya mwisho kabla ya kuzikwa Jumapili hii kijijini Qunu alikozaliwa. Baba yake, Mphakanyiswa Gadla Henry, mama yake Noqaphi Nosekeni na mwanae wa kiume Magkatho Lewanika Mandela walizikwa kwenye makaburi ya familia. Mandela aliomba azikwe jirani na familia yale.
Mamia ya watu walijitokeza katika barabara za mkoa wa Eastern Cape ambako Mandela atazikwa nyumbani Qunu
Takriban watu 5,000 wanatarajia kuhudhuria mazishi hayo Prince Charles wa Uingereza, Mwenyekiti wa tume Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, Rais wa zamani wa Zambia, Kenneth Kaunda, na mwanaharakati wa Marekani, Reverend Jesse Jackson.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Askofu Emeritus Desmond Tutu hatokuwepo kwenye mazishi hayo kwakuwa hakupewa mwaliko. Hata hivyo serikali imesema Tutu alingepiga simu kama angetaka kuhudhuria kwakuwa hakuna mwaliko wowote uliotumwa.
Watu walifurika barabarani angalau kumtupia jicho shujaa wao na kutoa heshima zao za mwisho.
Takriban watu 100,000 walitoa heshima zao za mwisho kwa Mandela mjini Pretoria siku ya Ijumaa kabla ya mamia ya wengine kukosa fursa hiyo pale walipokatazwa kumuona Mandela kutokana na ufupi wa muda.