Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

KIJANA AKUTWA AMEKUFA KWENYE KORONGO,LUBENGELA MKOANI KIGOMA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 


Polisi wakibeba mwili huo.
Kutokana na eneo alilokutwa marehemu kuwa na miundombinu mibovu ya kumtoa walilazimika kutumia ngazi,hivyo waliomba msaaada wa ngazi kwa gari la 'emegency' la Tanesco na hapa ngazi ilikuwa inashushwa tayari mwili kupandishwa juu kupelekwa eneo husika.



ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Katika hali ya kustajaabisha kijana mmoja alietambulika kwa jina moja la Yusuph (Me) mkazi wa Buzebazeba Ujiji amekutwa amekufa katika korongo la Lebengera jirani na Ofisi za CCM mkoa katika manispaa ya Kigoma Ujiji huku akiwa amejaa damu katika paji lake la uso

Mara baada ya Jeshi la Polis kufika eneo la tukio walimpekua marehemu na kumkuta na fedha taslimu kama elfu tatu hivi na karatasi ambayo haikujulikana maramoja imeandikwa nini
 tukio hilo limetokea Oktoba13 eneo tajwa hapo juu huku umati mkubwa ukiwa umefurika ili kumtambua na kushuhudia tukio hilo,

katika uchunguzi wa awali inasemekana tukio hilo limetokea usiku wa siku hiyo,kwani kutwa nzima ya siku hiyo hapakuonekana mtu ambae amekufa katika eneo hilo.

mmoja wa wananchi aliekuja kushuhudia tukio,na ambae ni mfanyakazi katika ofisi moja jirani na eneo la tukio( jina kapuni) amesema hii imekuwa ni mara ya pili kutokea tukio kama hili la mtu kukutwa ameuawa na kutupwa katika korongo hili,hivyo anaviomba vyombo vya usalama kuweka doria ya mara kwa mara eneo hili kwani eneo hili linakaribiana na Bar pamoja na Ofisi za Hazina Ndogo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>