Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MAREKANI YAPATA MGONJWA WA PILI WA EBOLA

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Mfanyakazi wa kituo cha afya aliyemtibu, Thomas Dancun kabla ya kifo chake katika jimbo la Texas nchini Marekani amepatikana na virusi vya ugonjwa wa Ebola.

“Tulijua kuna uwezekano wa kisa cha pili kuripotiwa ,na tumejitayarisha kwa uwezekano huo”alisema Daktari David Lakey ambaye ni kamishna wa idara ya afya katika jimbo la Texas”
Marehemu Dancun ambaye aliambukizwa ugonjwa huo nchini Liberia ,alifariki katika hospitali ya Dallas siku ya jumatano. Hata hivyo jina la mhudumu huyo halikutajwa.
Duncan alipatikana na virusi vya ugonjwa huo katika mji wa Dallas mnamo tarehe 30 mwezi Septemba ,siku kumi baada ya kuwasili kutoka katika ndege ya Monrovia kuelekea Brussels. Aliugua siku chache baada ya kuwasili nchini Marekani,na kuelekea katika hospitali ya Texas mjini Dallas akiwa na homa kali.
Lakini licha ya kuwaeleza madaktari kwamba alisafiri kutoka nchini Libya,aliagizwa kwenda nyumbani baada ya kupewa dawa za maumivu. Lakini Duncan baadaye aliwekwa katika karantini katika hospitali hiyo ,na kufariki baadaye licha ya kupewa dawa za majaribio.
Haijulikani iwapo afisa huyo aliyepatikana na virusi vya ugonjwa huo alikaribiana na Duncan au la baada ya kuonyesha dalili ama wakati alipolazwa hospitalini. Afisa huyo alipatikana na homa siku ya ijumaa kabla ya kuwekwa katika karantini ili kufanyiwa ukaguzi.

Source:BBC

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>