Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) YATOA ONYO NA KUKIPIGA FAINI KITUO CHA RADIO CHA TIMES FM

$
0
0
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 



KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo kali kwa kituo cha Redio cha Times Fm, pamoja na faini ya kulipa kiasi cha Sh milioni 1, kutokana na kukiuka vifungu vya maadili na kanuni za utangazaji, vilivyopo katika leseni ya utangazaji inayotolewa na mamlaka hiyo.

Akisoma hukumu hiyo jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margareth Munyagi, alisema ‘ Times Fm’ imepewa adhabu hiyo baada ya watangazaji wake kukiuka taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo, kwa kutangaza hewani maneno yanayokiuka maadili ya utangazaji.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Munyagi alisema kwa nyakati tofauti kupitia kipindi chake cha ‘Hatua tatu’ kilichorushwa saa 3 hadi saa 5 asubuhi na ‘Mitikisiko ya Pwani’, kilichorushwa mchana wa Agosti 29 mwaka huu, watangazaji wa vipindi hivyo walisikika wakizungumzia dondoo zilizolenga kuhamasisha ngono bila kuzingatia muda huo ambao watoto wengi wanaweza kusikiliza.

Alisema kiutaratibu muda ambao dondoo hizo zilikuwa zikitangazwa, si muda muafaka kwa kuwa vipindi hivyo pia vingewezwa kusikilizwa na watoto na kwamba muda wa dondoo kama hizo kutolewa unapaswa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri.

Aidha alisema utetezi uliotolewa na Mkurugenzi wa Redio hiyo, Leule Nyaulawa haukidhi haja mbali na kulipokea shitaka lililotolewa dhidi yao.

Nyaulawa alisema suala la kupata watangazaji wazuri Tanzania bado ni changamoto kutokana na vyuo vingi kuzalisha watangazaji wasio na uwezo mzuri.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>