Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepokea mwili wa Marehemu Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario (Mstaafu) kutoka nchini India leo tarehe 09 Oktoba, 2014 katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl JK Nyerere Dar es salaam,mwili wa marehemu umewasili kwa Shirika la ndege la Ethiopia saa 7:30 mchana.
Mwili wa marehemu utaagwa kesho tarehe 10 Oktoba, 2014 saa 4:00 asubuhi katika viwanja vya hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na baadaye mwili utasafirishwa kwenda kwao Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Oktoba, 2014 saa 7:00 mchana siku ya Jumamosi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Dkt Hussein Mwinyi anatarajiwa kuongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
MEJA JENERALI MUHIDINI KIMARIO (MSTAAFU)
AMINA
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi,
Upanga
S.L.P 9203,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi,
Upanga
S.L.P 9203,
Dar es Salaam,
Tanzania.